HISTORIA YA KAMPUNI YA UJENZI SUMAJKT CONSTRUCTION COMPANY LIMITED
1. Kabla ya kusajiliwa kama mkandarasi, JKT ilitekeleza shughuli za ujenzi kupitia “building brigade”kuanzia mwaka 1969 hadi 1972.
2. Katika kutekeleza majukumu yake “brigade” ilitumia wataalamu wa fani mbalimbali waliopata mafunzo ndani na nje ya nchi. Kazi kubwa iliyotekelezwa na “brigade” ya Ujenzi ni ujenzi wa Makambiya Jeshi la Kujenga Taifa na kushiriki katika ujenzi wa nyumba za kupangisha za “National House Corporation” katika mradi uliojulikana kama “Slum Clearance Scheme” kuanzia mwaka 1968-1973 katika maeneo ya Magomeni na Kinondoni.
3.Shughuli za Ujenzi ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa zilitambuliwa rasmi na Wizara ya Ujenzi baada ya kukidhi mahitajio yote ya mkandarasi na kusajiliwa katika hatua mbalimbali kama ifuatavyo:-
a. Wizara ya Ujenzi ilisajili shughuli za ujenzi ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa mwaka 1972 na jina likabadilika kutoka “Builders Brigade” kuwa “National Service Construction Department”.
b. “National Service Construction Department” ilisajiliwa kama Mkandarasi daraja la tatu ”Building Contractor” Januari 1998, baada ya kuanzishwa Bodi ya Makandarasi mwaka 1997.
c. Mwaka 2004 baada ya kutekeleza kwa ufanisi Mradiwa Ujenzi wa Nyumba 150 za Watumishi wa Serikali huko Mbweni Dar es Salaam “National Service Construction Department” ilipandishwa daraja ”Building Contractor” kutoka daraja la tatu kuwa la kwanza.
d. (1) Mwaka huohuo 2004 NSCD ilipata usajili wa kandarasi wa Ujenzi wa Barabara daraja la nne “Civil Works Contractor Cass Four” na Utandazaji wa Umeme daraja la Nne “Electrical Contractor Class Four”.
(2) Mwaka 2019 SUMAJKT CCL ilipanda daraja Ukandarasi wa Ujenzi wa Barabara daraja la tatu“Civil Works Contractor Cass Four”
e. Jitihada za SUMAJKT kupitia kampuni tanzu ya ujenzi NSCD imebadili jina lake kutoka “National Service Construction Department” na kuwa “SUMAJKT CONSTRUCTION COMPANY LIMITED” taratibu za kubadili toka “BRELA” zilikamilika tarehe 24 Novemba 2018. Kazi ya kuwajulisha wadau na kupitia matangazo kwenye vyombo vya habari zimefanyika juu ya matumizi ya jina jipya.
KUSAJILIWA KAMA WATAALAMU WA SHAURI
4. “SUMAJKT Construction Company Limited” mbali na kusajiliwa kama mkandarasi tajwa hapo juu imepata Usajili wa washauri wataalamu katika fani zifuatazo:-
a. Usanifu Majengo (Architectural Firm) kuanzia tarehe 22 Desemba 2017 kwa nambaya usajili APL 268:306.12/17.
b. Wahandisi Washauri (Consulting Engineers) kuanziatarehe 19 April 2018 kwa namba ya Usajili 207.
c. Wakadiriaji majenzi (Quantity Surveying Firm) kuanzia tarehe 25 Sep 19 kwa namba ya Usajili QPL 146.190.9/19.